Tayarisha muziki ukitumia Google Flow Music
Google Flow Music inakupa uwezo wa kutumia mifumo ya AI ya muziki inayoongoza kutoka Google kwa haraka. Iwe unaandika wimbo wako wa kwanza au unavumbua aina mpya kabisa ya muziki, Google Flow Music inakupa udhibiti kamili kwa urahisi.
ANZA KWA KUANDIKA KIDOKEZO
Furahia uwezo halisi wa kutayarisha muziki wenye ubora wa juu. Anza kwa maneno ya wimbo au wimbo rahisi wa ala ya muziki, kisha uboreshe sauti yako kwa njia endelevu na haraka ukitumia vidhibiti vya kina vya ubunifu vinavyoendeshwa na Gemini. Iombe tu Producer "iongeze besi" au "iimbe maneno ya wimbo kwa sauti nzito" ili uweke madoido maalum ya sauti na utayarishe nyimbo zenye urefu kamili.
ANDAA MSETO WA SAUTI
Pakia nyimbo zako, badilisha sauti, vaibu na mengineyo. Andaa miseto yake ukitumia Matoleo Mengine ya Nyimbo, Badilisha na Refusha ili uboreshe sauti yako.
BUNI SPACES
Buni chochote unachotamani kwa kutumia Spaces. Buni programu jalizi maalum za sauti, michezo ya muziki au DAW zilizowekewa mapendeleo. Nafasi yako, msimbo wako. Tuma programu zako ndogo ili zitumike na zibadilishwe na jumuiya pana.
VIDEO ZA MUZIKI
Elekeza video zako za muziki. Tumia mfumo mpya kabisa wa video wa Veo ili uhuishe sauti yako moja kwa moja pamoja na wimbo wako. Unadhibiti wahusika, mitindo na vipengele vyote.
TUMA UNACHOBUNI
Tayarisha orodha, chapisha nyimbo zako, fuatilia wasanii unaowapenda na ugundue muziki mpya kila siku. Google Flow Music hujifunza mitindo unayopendelea na inazidi kuboreshwa kadiri unavyoendelea kuitumia. Kadiri unavyotayarisha, ndivyo inavyoelewa zaidi mapendeleo yako binafsi ya sauti.
Utatayarisha nini leo?
Sheria na Masharti: https://policies.google.com/terms
Sera ya Faragha: https://policies.google.com/privacy
Ilani ya Faragha: https://www.flowmusic.app/privacynotice
Tayarisha nyimbo, elekeza video za muziki, simba ala na mengineyo.
Ilisasishwa tarehe
23 Okt 2026